Ommy Dimpoz Amuweka wazi Mchumba wake....Jionee Live hapa Walivyotokelezea
![]() |
Picha aliyopost Ommy Dimpoz ikiashiria kuwa huyo ndiye mpenzi wake
|
Msanii Ommy Dimpoz ambaye anafanya vyema na wimbo wake 'Kajiandae' wiki kadhaa zilizopita alifunguka na kusema ikifika wakati ataweka wazi suala la mahusiano yake kwa jamii, na kumuweka wazi mchumba wake ili watu wajue.
Ommy Dimpoz alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz cha EATV wiki kadhaa
zilizopita, Ommy alifunguka na kuthibitisha kuwa kwa sasa yupo kwenye
mahusiano na raia wa China., ambaye watu wengi hawamjui.
Juzi Ommy Dimpoz ametupia Instagram picha ya pamoja akiwa na binti huyo
mwenye asili ya China kisha akaweka 'emoji' yenye ishara ya love,
akiashiria 'Mapenzi bampa 2 bampa'.
Ingawa Ommy Dimpoz hakutaka kufungua mjadala kwenye picha ile kwa kuamua
kufunga uwanja wa comment ili watu wasiweze kuzungumza wala kujadili
katika picha hiyo. Lakini ukweli ni kwamba picha ile inazungumza mambo
mengi kwa kila anayeiangalia.



