Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amedai kitendo
cha Baraka The Prince kumsaini aliyekwa member wa kundi la Weusi Lord
Eyez itakuwa ni safari ya kipofu na kiziwi.
Miezi michache iliyopita Baraka Da Prince alitangaza kutaka kumsaini
Lord Eyez huku uongozi wa Weusi ukidai hauna taarifa hizo na wao
wanazisikia tetesi hizo kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumzia suala hilo katika 255 ya XXL ya Clouds FM, rapper Nay wa
Mitego amedai kati ya Barakah na Lord Eyez haoni wa kumuongoza
mwenzake.
“Hiyo ni safari ya kipofu na kiziwi, naweza kusema hivyo. Kiukweli
haimake sense, kwasababu mtu ambaye anataka kuongozwa na yeye
akamuongoza mwenziye ndio maana ya mfano wangu. Kibaya zaidi Lord Eyez
ni mkubwa zaidi ya Baraka. Sawa kuna watu ambao wanasimamiwa na watu
wadogo lakini ukiangalia pale alipo msanii kama Baraka anahitaji msaada
zaidi.”
Suala hilo limeleta mjadala katika mitandao ya kijamii huku wengi wakiendelea kusubiri kuona itakuwaje.
Umeisikia Hii????Nay wa Mitego anadai Barakah The Prince kumsaini Lord Eyez ni safari ya kipofu na kiziwi
Reviewed by Mipiko
on
11:29 AM
Rating: 5