TTCL yaondoa changamoto ya Dawa kituo cha Afya cha Tandale
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri W.Kindamba akikabdhi msaada wa dawa
na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Tandale kwa Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto na kushuhudiwa
na Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Ally Hapi.
Mkuu
wa Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Ally Hapi akizungumza kwenye hafla ya
kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba kutoka Kampuni ya Simu
Tanzania(TTCL). Katika Haflya hiyo ilihudhuriwa na Kaimu Afisa Mtendaji
Mkuu, Bw Waziri W.Kindamba, Dr Zuhura Majapa Mratibu wa BRN Manispaa ya
Kinondoni na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tandale Dkt Emmanuel
Kazimoto.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri W.Kindamba akizungumza kwenye hafla
ya kukabidhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa Kituo ch Afya cha Tandale,
wilayani Ilala, jijini Dar es salama
Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali
katika kutatua changamoto katika sekta mbali mbali nchini ili kuboresha
huduma za Kijamii zinazogusa maisha ya kila siku ya Wananchi kwa lengo
la kuyaboresha na kuongeza kasi ya Nchi kupiga hatua za Maendeleo.
Ahadi
hiyo imetolewa Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL
Bw Waziri Kindamba alipokuwa akikabidhi msaada wa dawa na vifaa tiba
kwa Kituo cha Afya cha Tandale, kilichopo Wilaya ya Kinondoni, mkoa wa
Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii.
Msaada
huo umekabidhiwa kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Tandale Dkt
Emmanuel Kazimoto, tukio lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni
Mheshimiwa Ally Hapi ambaye ndie aliwezesha kupatikana kwa vifaa hivyo
kupitia program yake maalumu ya kuwasiliana na Taasisi za Umma na
Binafsi ili zisaidie kuboresha huduma za kijamii Wilayani kwake.
Akizungumza
kwenye hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Kituo hicho, Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameishukuru Kampuni ya Simu TTCL kwa
msaada iliotoa na kubainisha kuwa, msaada wa dawa na vifaa tiba
utasaidia sana kuboresha huduma katika kituo hicho chenye kuhudumia
idadi kubwa ya Wananchi wa kipato chini.
“Juhudi
hizi za kusogeza huduma kwa wananchi ni muhimu sana katika kipindi hiki
ambacho serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu Dkt John
Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha maisha ya watu wa hali ya chini na
kuwaondoa katika unyonge unaowafanya kushindwa kutoa mchango stahiki
katika jitihada za nchi kujiletea Maendeleo” Amesema Mhe Hapi
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Tandale
kuhakikisha kuwa unasimamia vyema matumizi ya dawa hizo ili zitumike
kwenye malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kuboresha huduma kwa Wananchi.
Naye
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri W.Kindamba amesema, TTCL
imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Jamii kwenye sekta mbalimbali
kama vile elimu, afya, michezo, matumizi ya teknolojia ya Habari na
Mawasiliano, makundi maalum na wakati wa maafa.
“TTCL
imetoa msaada huu wenye thamani ya shilingi milioni 5, dawa zilizotolewa
ni pamoja na Paracetamol Syrup, Paracetamol Tabs, Diclofenac,
Amoxicillin, Amoxicillin Granules, Folic Acid, Gloves Surgical, Bandage,
Magnesium Trisilicate, Methylated Spirit na nyinginezo nyingi.
Tunaamini kuwa msaada huu utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na
utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa dawa kwenye kituo hiki”
amesema Waziri K.Kindamba.
Aidha,
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri W.Kindamba ametoa rai kwa
taasisi na makampuni mengine kukusaidia juhudi za Serikali katika
kusaidia huduma za Kijamii hali itayoimarisha uhusiamo mwema na Wananchi
na kutoa suluhisho kwa changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo
mbali mbali nchini.


