Serikali imetakiwa kupiga marufuku pombe kali zinazofungwa kwenye
pakiti maarufu viroba, ili kuwanusuru vijana na ulevi unaosababisha
Taifa kupoteza nguvu kazi.
Mkurugenzi wa kituo cha wagonjwa wasiojiweza cha Bashay wilayani Mbulu,
Mkoa wa Manyara, Padri James Amnaay alitoa rai hiyo juzi alipopokea
msaada wa vyakula, nguo na sabuni kutoka Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT)
wilayani hapa.
Padri Amnaay alisema iwapo Serikali itapiga marufuku pombe hizo,
itasaidia vijana kutojiingiza kwenye ulevi ambao umekithiri na
kusababisha baadhi yao kuwa vichaa.
Alisema kutokana na urahisi wa kubeba na bei nafuu, pombe hizo
zimewaathiri vijana wengi wanaokunywa na kulewa hatimaye kujiingiza
kwenye dawa za kulevya.
Serikali Yashauriwa kupiga Marufuku viroba
Reviewed by Mipiko
on
7:44 PM
Rating: 5