JUBILEE YAUNGA MKONO KEN LUSAKA NA JUSTIN MUTURI KUWA MASPIKA
Mrengo wa Jubilee sasa umempendekeza rasmi aliyekuwa gavana wa Bungoma Ken Lusaka kuwa spika wa bunge la senate na Justin Muturi kusalia spika wa bunge la kitaifa.
Kwenye mkao ikulu ulioongozwa na kinara wa Jubilee Uhuru Kenyatta baadhi ya viongozi wenye ushawishi walipendekezwa kuongoza mabunge yote mawili ikiwa ni katika azma ya kusukuma ajenda ya Jubilee na kwa pakubwa kuwapongeza waliofanya Jubilee kupataa uungwaji mkono zaidi.
Haya yalijiri huku wabunge wanaoegemea mrengo wa Nasa wakikubaliana kwa pamoja kuhudhuria shughuli ya kuapishwa hiyo kesho wakiapa kufanya kazi pamoja.