ASKOFU GWAJIMA AIBUKA NA SAKATA LA TUNDU LISSU...ASEMA JUMAPILI HII DUDE LITAAMSHWA LIVE
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amevunja ukimya kufuatia sakata la kushambuliwa kwa Mbunge Tundu Antiphas Lissu ambaye amejeruhiwa kwa risasi kadhaa jana mchana.
Kupitia akaunti ya insta Askofu Gwajima leo ameitaarifu jamii kuwa Jumapili hii ya tarehe 10 Septemba kutakuwa na maombi maalumu ya kuiombea afya ya Mbunge huyo wa Singida Mashariiki Tundu Lissu.
Aidha akofu Gwajima ameawaalika wananchi hususani wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuungana kwa pamoja katika kanisa la Ufufuo na uzima lililopo Ubungo ili kufanikisha maombi hayo.
Tundu Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS jana Alhamisi alipigwa risasi wakati akielekea nyumbani kwake Dodoma na mpaka hivi sasa hali yake kiafya inaarifiwa kuwa haijatengamaa na anaendelea na matibabu jijini Nairobi nchini Kenya.