Juma
Kaseja amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kusema atakapostaafu kucheza
soka ataingia rasmi katika kiwanda cha utangazaji, ambapo awali ataanza
kwa kutumia kipaji chake lakini kadri siku zinavyozidi kwenda itabidi
aingie shule ili kuwa mtangaji mzuri zaidi na bora.
"Kila kitu kinahitaji elimu,
ila mimi kwanza nitaanza hivi hivi nilivyo halafu kadri nitakavyozidi
kwenda nitakuwa najiendeleza na shule ili niwe mtangazaji mzuri" alisema Juma Kaseja
Mbali na hilo Juma Kaseja amesisitiza wachezaji wadogo wanaokuja
kwenye soka wanapaswa kuwa wavumilivu, wasikivu kwa walimu wao na kuwa
na nidhamu kama wanapokuwa kwa wazazi wao.