RC Mwanri atoa onyo kwa watu wanaounganisha sauti yake ‘Soma Hiyoo’ na sauti ya Rais Magufuli (+video)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri amewataka Waandishi wa Habari na watu wa mitandaoni wanaounganisha suti yake na kuchanganya sauti ya Rais Magufuli, kuacha mara moja tabia hiyo kwani inaleta picha mbaya kwa viongozi.
Mwanri akiongea na Bongo5 amesema kuwa kitendo hicho sio kizuri, kwani viongozi wa juu kama Rais ni taasisi na mamlaka yake ni kubwa.