Irene Uwoya afunguka kuhusu wanaume wenye sura mbaya...Adai akiwaona tu Hisia zake za Mapenzi Zinapanda kwa kasi

Kwa mujibu wa Irene, wanaume wenye sura mbaya ndio ambao huamsha zaidi hisia zake za kimapenzi! Strange, lakini ndio ukweli wake. Muigizaji huyo ambaye ameandaa event maalum kwaajili ya Valentine’s Day aliyoipa jina, ‘Irene Uwoya Valentine’s Special Night, ameahidi kueleza baadhi ya mambo ambayo watu hawafahamu kuhusu yeye katika sekta ya malavidavi.
“Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa sijawahi kuvutiwa na wanaume wenye mionekano mizuri, sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI,” ameandika Uwoya.
Wanaume wenye sura nzuri, poleni!


