Breaking News

Kenya yatangaza ukame kuwa janga la taifa


Serikali ya Kenya imetangaza hali ya ukame iliyoko sasa iliyoathiri kaunti 23 zenye ukame na baadhi ya maeneo mengine kuwa ni janga la taifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka wadau wote kuiunga mkono serikali kwa kuongeza miradi ya kukabiliana na ukame ambao umewaacha watu zaidi ya milioni 2 wakihitaji msaada wa dharura wa chakula. Amesema kuungwa mkono na wedau hao kutasaidia juhudi za serikali katika kudhibiti madhara ya ukame.

Rais Kenyatta pia ametoa wito kwa wadau wa ndani na nje ya nchi kuungana na kusaidia juhudi za serikali kudhibiti hali hiyo ambayo sio tu inaathiri binadamu na wanyama, lakini pia inaathiri wanyamapori.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limeonya kuwa Kenya inakabiliwa na hali mbaya ya ukame unaosababisha uhaba wa chakula.