Alichokisema Baba Diamond Kuhusu Nani Mkali Kati ya Mwanae Diamond na Darasa.

Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Jumaa
amefunguka kuwa Mwanamuziki, Shariff Thabeet ‘Darassa’ licha ya watu
kusema yupo juu lakini hawezi kumshinda au kufikia levo alizopo mwanaye.
Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, baba Diamond alisema licha ya watu
wengi kuvutiwa na Wimbo wa Muziki wa Darassa lakini hawezi kumshinda
mwanaye huyo kwa sababu ni wimbo huo mmoja tu ndiyo uko kwenye chati
kitu ambacho ni tofauti na Diamond ambaye anazo nyingi zinazofanya
vizuri.
“Diamond ni mpiganaji sana na ana mbinu nyingi kwenye suala zima la
muziki wake ndiyo maana kila siku anazidi kuwa juu na kujulikana mataifa
mbalimbali, wanaosema Darassa atampita au kumfikia Diamond alipo
wanajidanganya, hawezi hata kwa nusu yake,” alisema baba Diamond


