Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Bw. Antonio Guterres amempongeza waziri mkuu wa zamani wa serikali ya
mpito ya Somalia Bw. Mohammed Abdullahi Mohammed kwa kuchaguliwa kuwa
rais wa Somalia na kumtaka aunde serikali shirikishi haraka
iwezekanavyo.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu mkuu huyo imesema, Bw.
Guterres amesema serikali mpya na wajumbe wa shirikisho wanapaswa
kukabiliana na masuala ya dharura ya nchi hiyo kwa pamoja, ikiwemo
kutunga katiba na kuunda jeshi la ulinzi la taifa.
Amesema hivi sasa Somalia inakabiliwa na ukosefu wa chakula
uliotokana na ukame, na Umoja wa Mataifa unapenda kutoa msaada kwa
Somalia.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amtaka rais mpya wa Somalia aunde serikali shirikishi haraka iwezekanavyo
Reviewed by Mipiko
on
9:41 AM
Rating: 5