Rais Xi Jinnping wa China leo
amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Donald Trump wa Marekani,
na kumshukuru kwa salamu zake za Sikukuu ya Taa na Mwaka Mpya wa Jadi wa
Kichina kwa wananchi wa China.
Katika mazungumzo hayo, rais Xi pia amemsifu rais Trump kwa lengo
lake la kupanua ushirikiano kati ya China na Marekani na kukuza uhusiano
wa kiujenzi kati yao unaonufaisha nchi hizo mbili na jumuiya ya
kimataifa. Pia amesifu msimamo wa rais Trump kuhusu sera ya China moja.
Kwa upande wake, Rais Trump amesema, ni muhimu sana kudumisha
mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili, na kusisitiza kuwa
serikali ya Marekani itashikilia sera ya kuwepo kwa China moja.
Marais wa China na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu
Reviewed by Mipiko
on
9:32 AM
Rating: 5