Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas Texas Marekani leo ambapo kwenye list yote Watanzania walioshinda ni watatu.
Watanzania walioshinda ni Dj D Ommy wa CloudsFM kupitia show mbalimbali ikiwemoXXL na AMPLIFAYA ambapo ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika, mwimbaji Harmonize akishinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 huku Diamond Platnumzakishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.
Sasa miongoni waliotoa pongezi kwa
Harmonize ni Diamond Platnumza ambae kupitia instagram alipost picha na
kuyaandika haya>>>>hii picha inanikumbusha mwaka jana ulipokuja nipokea airport kutokea@afrimma …ukaniuliza “hivi ipo siku nami nitachaguliwa tunzo yoyote ya kimataifa”….nikakwambia “Ukifanya kazi kwa bidii’
‘Ukimuheshimu
kila mtu, ukamuamini na kumuomba Mwenyezi Mungu basi Mollah
atakufungulia ndoto zako….na leo hii kweli Tunafurahia Ushaindi wako wa
Msanii Bora Chipkizi Africa….. Hongera sana @harmonize_tz na shukran sana sana kwa Mashabiki zetu pendwa kwa kura na @Afrimma kwa kuendelea kuvinyanyua vipaji vya Africa’-Diamond Platnumz
Maneno ya Diamond kwa Harmonize baada ya kushinda tuzo ya AFRIMMA
Reviewed by Mipiko
on
2:23 AM
Rating: 5