Breaking News

Ufaransa yatishia kuiwekea vikwazo DRC


                       Rais Joseph Kabila wa DRC


Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ,Joseph Kabila ni sharti aheshimu katiba na kujiuzulu mwishoni mwa muhula wake ,waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Mark Ayrault amesema katika mahojiano na kituo cha habari cha TV5.

Bwana Ayrault alikuwa akisisitiza wito aliotoa wiki iliopita wakati akiwahutubia wanafunzi mjini Paris.

Wakati huu aliangazia madai kwamba Ufaransa imekuwa ikiingilia maswala ya ndani ya DRC,akisema kuwa taifa lake haliko pekee kumkumbusha Kabila kwamba lazima aheshimu sheria.

Aliambia kituo hicho:''Rais Kabila lazima aonyeshe mfano .Ni lazima aheshimu katiba.Iwapo vikwazo vitahitajika tutaamua kuvitekeleza.Nataka watu waelewe; Watu waliopo katika mamlaka DRC ni lazima wawajibike.Iwapo wanahitaji amani nchini mwao,iwapo wanajali hali ya watu wao ,ni lazima wafuate katiba''.