Benki ya Dunia imesema sera za serikali zimewasaidia maskini kujiinua
Tanzania imetajwa
na Benki ya Dunia kuwa miongoni mwa mataifa machache duniani ambayo
yamefanikiwa pakubwa kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini.
Kwenye
ripoti ya benki hiyo kuhusu usawa duniani, Tanzania imeorodheshwa
pamoja na Cambodia na Brazil kama nchi tatu zilizopiga hatua sana.
Nchini
Tanzania, ripoti hiyo inasema, ufanisi ulipatikana katika kipindi
ambacho taifa hilo lilipata ukuaji thabiti wa uchumi wa kiwango cha
wastani cha asilimia 6.5 kila mwaka kati ya 2004-2014.
"Kiwango
cha umaskini kitaifa kilishuka kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi
asilimia 28.2 mwaka 2012," ripoti ya benki hiyo inasema.
Kwenye
kipimo cha pengo kati ya maskini na matajiri, Tanzania iliimarika kutoka
alama 39 mwaka 2007 hadi chini ya alama 36 mwaka 2012.
Kipimo cha wastani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara mwaka 2015 kilikuwa alama 45.1.
"Hatua
zilizopigwa na Tazania katika kupunguza pengo kati ya maskini na
matajiri kipindi hiki kifupi ni cha kutia moyo," Benki ya Dunia inasema.
Takwimu muhimu kuhusu Tanzania
6.5%
Kiwango cha wastani cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania 2004 hadi 2014
28.2 % Kiwango cha umaskini kitaifa kufikia mwaka 2012
"Ushahidi unaonesha ufanisi huu ulitokana sana na ongezeko la matumizi miongoni mwa watu wa tabaka la chini."
Miongoni
mwa asilimia 40 maskini, matumizi yaliongezeka kwa asilimia 3.4
ikilinganishwa na asilimia 60 wenye pesa ambao ongezeko lao la matumizi
lilikuwa asilimia 1 pekee.
"Ni wazi kwamba mambo yaliwaendea vyema zaidi watu maskini kuliko matajiri kipindi hiki," ripoti hiyo inasema.
Kuanzia
mwaka 2007, kulikuwa na ongezeko katika biashara ya rejareja na
viwanda, hasa vya vyakula, vinywaji na tumbao jambo ambalo benki hiyo
inasema liliwezesha watu wasio na ujuzi sana kushiriki katika uchumi.
Kujitolea
kwa serikali katika kuendeleza sera ambazo zinalenga kusawazisha mapato
pia kumechangia Tanzania kupiga hatua, benki hiyo inasema.
Uchumi wa nchi za Afrika washuka hadi asimia 1.6
Moja
ya sera hizi ni mkakati wa serikali wa kuimarisha kupatikana kwa huduma
za msingi kama vile afya, elimu ya msingi, maji na usafi miongoni mwa
watu maskini.
Pili ni Mfuko wa Maendeleo wa Tanzania ambao benki
hiy inasema umesaidia jamii maskini kuweka akiba na kuwekeza hasa katika
mifugo.
Hata hivyo, benki hiyo imesema Tanzania inafaa kufanya
juhudi zaidi kupunguza tofauti kati ya mikoa pamoja na kuimarisha
upatikanaji wa huduma za kimsingi. Juhudi zaidi zinahitajika katika
upatikanaji wa umeme na huduma za usafi.
Tanzania yasifiwa na Benki ya Dunia kwa kuhakikisha usawa
Reviewed by Mipiko
on
12:42 AM
Rating: 5