Kaimu meneja wa mradi wa maji awekwa ndani kwa saa 48
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo amesema ni jambo la kusikitisha kuona viongozi waliopewa dhamana na serikali wanakuwa sehemu ya kuhujumu umma ikiwa ni pamoja na kuzuia maji kwenda kwa wananchi na badala yake kuyaelekeza kwa wafanyabiashara wa maji kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.
Akijitetea baada ya kutolewa ndani ya kituo cha Polisi meneja wa mamlaka ya maji Makonde Athumani Semkondo amekiri kuwapo kwa hujuma hiyo ambayo amesema huenda ilifanywa na watendaji wake wa chini pasipo yeye kujua.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya anasema sehemu kubwa ya tatizo la maji katika wilaya ya Newala linasababishwa na urasimu, madhaifu ya viongozi na watendaji kutosimamia maadili ya kazi zao.


