Baada ya Aishi Manula kusaini
mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba, klabu ya Azam imemnasa
golikipa wa Mbao FC Benedict Haule na kumsainisha mkataba wa miaka
miwili ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manula.
Haule amepata umaarufu baada ya kusimamishwa kwa aliyekua golikipa
namba moja wa Mbao Musa Ngwegwe. Haule alifanya vizuri kwenye mechi
alizosimama golini kuelekea mwisho mwa msimu na kuisaidia timu yake
kukwepa kushuka daraja huku akiifikisha fainali ya Azam Sports
Federation Cup.
Mechi kati ya Mbao dhidi ya vigogo vya soka nchini (Simba na Yanga)
zilimpa jina baada ya kuonesha kiwango cha juu. Licha ya kupoteza mchezo
kwa mabao 3-2 mbele ya Simba, kipa huyo alikuwa kwenye kiwango bora.
Alionesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Yanga
na kuiongoza Mbao kushinda kwa goli 1-0 ushindi ambao uliwahakikishia
kubaki kwenye ligi kuu kwa ajili ha msimu ujao.
Simba watamkumbuka Haule kwa kile alichokifanya kwenye uwanja wa
Jamhuri Dodoma siku ya mechi ya fainali ya Azam Sports Federation Cup
ambapo Simba ilishinda kwa magoli 2-1 na kuchukua taji hilo lililowapa
fursa ya kucheza michuano ya CAF Confederation Cup msimu ujao.
KIPA WA MBAO FC ASAINI MKATABA MNONO KUZIBA NAFASI YA AISHI MANULA WA AZAM FC
Reviewed by Unknown
on
9:23 AM
Rating: 5