Makamba amwaga mifuko 100 ya sementi Katurukila

Akiwa katika kijiji hicho, kilichopo Tarafa ya Mang'ula Makamba alisema amefurahishwa na mwamko waliokuwa nao wakazi wa Katurukila wa kutunza mazingira bila kushurutishwa
"Hivi mnaweza kuniambia mnataka zawadi gani?Akajitokeza mwanakijiji mmoja Amir Mwema na kusema Mheshimiwa (Makamba) kituo chetu cha afya hakipo katika hali nzuri tunaomba utusaidie.
Makamba alikubali ombi hilo na kuwaahidi mifuko hiyo itakwenda Katurukila baada ya wiki moja


