Afande Sele ndio kajiunga CCM? kayaongea haya

msanii mkongwe kutoka Bongoflevani, Afande Sele ameingia kwenye
headlines za mitandao kuhusu kuhamia CCM kutokana na picha iliyosambaa
ikimuonesha akiongea kwenye msafara uliosimamishwa na Makamu wa Rais
Samia Suluhu mkoani Morogoro.
Afande Sele amepetikana na kuongea haya - Hizo taarifa si kweli na
napokea simu nyingi sana kuhusu habari uliyoisikia ile siku nilipata
mualiko wa Serikali kuzungumza machache baada ya Makamu wa Rais mama
yetu Samia Suluhu alipofika mkoani kwetu sikuwa pekee yangu bali
nilikuwa na mkuu wa mkoa naomba watu wajue kwamba mimi bado nipo katika
chama changu cha ACT’


