Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey Polepole amewapiga
marufuku wajumbe wa mashina na viongozi wengine wa CCM kujihusisha na
uidhinishaji mauzo ya ardhi, huku akiwataka wananchi kuwa makini na
kufuata utaratibu wa kisheria wakati wa ununuzi.
Polepole alitoa onyo hilo jana wakati wa mkutano na wakazi wa King’azi
Juu, Kata ya Kwembe, baada ya kuelezwa kuwa wana matatizo mengi ya ardhi
yanayotokana na baadhi viongozi kuuza eneo kwa mtu zaidi ya mmoja.
Wananchi hao walimweleza kuwa, udanganyifu unaofanyika unatokana na
baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa na wajumbe wa mashina wa CCM
kula njama na wamiliki wa maeneo, kuuzia watu eneo moja zaidi ya mara
moja.
Polepole alisema CCM ipo kwenye harakati za kujijenga, hivyo lazima
kumaliza migogoro hiyo kama sehemu ya kujirekebisha. Mwenyekiti wa mtaa
huo, Seleman Bheho alisema mwaka 2014/15 alipoingia madarakani .ofisi
yake ilikuwa akipata kesi za za ardhi nane mpaka 10 kwa siku, lakini
sasa zimepungua hadi tatu kwa wiki.
DC Polepole awakunjulia ‘makucha’ viongozi CCM
Reviewed by Mipiko
on
6:56 PM
Rating: 5