SPIKA WA BUNGE ATUMA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA WANAFUNZI 32 ARUSHA.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo kufuatia vifo vya wananafunzi, walimu na dereva
wa Shule ya Msingi Lucky Vicent, baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kupata ajali jana asubuhi katika eneo la Rhotia Marera, wilayani Karatu
mkoani Arusha.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya
ajali iliyogharimu maisha ya watoto wetu, hakika hili ni pigo kwa Taifa
zima, namuomba Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” alisema Ndugai na kuongeza:
“Natoa
pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao,
Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu,
vilevile nawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapate uponyaji wa
haraka.”