MTOTO WA MIAKA 12 AUAWA KISHA KUNYOFOLEWA MACHO NA sSEHEMU ZA SIRI
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtoto wa miaka 12, Dorcas Meshak mkazi wa
kitongoji cha Mbughantigha kijiji cha Matongo tarafa ya Ikungi, ameuawa
na watu wasiojulikana na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake.
Akizungumza
kuhusu tukio hilo, Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa, SSP Isaya
Mbughi alisema tukio hilo lilitokea Mei, 18 mwaka huu saa sita mchana
wakati ambao Dorcas alipoondoka nyumbani kwao kwa lengo la kwenda
shambani kuchuma mahindi, umbali wa kilometa 70.
Alisema mtoto huyo amenyofolewa macho yote mawili, kukatwa matiti yote na kuondolewa sehemu zake za siri.
“Mtoto
Dorcas hakuweza kurudi nyumbani kitendo kilichosababisha ipigwe yowe
ili watu wakusanyike kwa ajili ya kumtafuta. Haikuchukua muda mrefu,
mwili wa Dorcas ulikutwa ukiwa umenyongwa hadi kufa kwa kamba ya ngozi,”
alisema.
Alisema
uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji hayo yanahusishwa na imani za
ushirikina na hadi sasa hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na mauaji
hayo.
Katika
tukio la pili, Kaimu Kamanda Mbugh, alisema watu wawili wamepoteza
maisha kufuatia kutokea ajali ya gari anina ya Noah, tukio ambalo
lilitokea Mei, 20 mwaka huu saa 6.45 mchana huko katika kijiji cha Mwaja
tarafa ya Unyankumi Manispaa ya Singida.
“Ajali
hiyo imehusisha noah T.402 DFH iliyokuwa ikiendeshwa na Said Shaban
(33), na chanzo cha ajali ni mwendo kasi kitendo kilichosababisha
ashindwe kulimudu. Waliofariki kwenye ajali hiyo,ni Elia Daniel (34)
mkulima kijiji cha Mwankoko na mwanamke mmoja ambaye jina wala makazi
yake,hayajafahamika,” alisema.
Aidha,
aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Mratibu Elimu kata ya Mtamaa,
Nicodem Elias (45), Juma Ramadhan, mwalimu Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi, Elia Bilau mkulima na mkazi wa Magungumka Kapela Donad (28).
Kaimu
kamanda huyo, alisema dereva wa Noah hiyo Said Shaban anashikiliwa na
Jeshi la Polisi na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazomkabili.