KOREA KASKAZINI KAMA KAWAIDA YAKE....YAFANYA JARIBIO LINGINE LA KOMBORA AMBALO LILIPAA KILOMITA 500
Shirika la habari la taifa nchini humo KCNA lilisema kuwa zana hiyo sasa iko tayari kutumiwa kwa shughuli za kijeshi.
Ikulu
ya White House ilisema kuwa kombora hilo lilikuwa la masafa marefu
kuliko makombora yaliyotumiwa na Korea Kaskazini wakati wa majaribio
matatu ya awali.
Jaribio
hilo linakuja wiki moja baada ya Korea Kaskazini kufanyia jaribio la
kile ilichokitaja kuwa kombora jipya lenye uwezo wa kubeba silaha za
nuklia.
Jumatatu iliyopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa Korea haistahili kufanya majaribio zaidi.
Sasa
baraza hilo linatarajiwa kukutana kwa faragha siku ya Jumanne kwenye
mkutano ulioitishwa na Marekani, Korea Kusini na Japan.
Wizara
ya mashauri ya nchi za kigeni ya Korea Kusini imelitaja jaribio hilo
kuwa la kiholela huku waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani
akilitaja kuwa la kughadhabisha.
Kombora
hio lilisafiri umbali wa kilomita 560 kuelekea bahari ya Japan. Kombora
la wiki iliyopita lilisafri umbali wa kilomita 700.