MKURUGENZI WA CLOUDS MEDIA GROUP AFUNGUKA KUHUSU KAULI ZILIZOTOLEWA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM LEO HII
Ruge
ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na
kituo hicho, ambapo walikuwa na kipindi cha ‘SHUKRANI’ kwa wasikilizaji
wao na watu waliowahi kuwasaidia kupata misaada.
“Kila
mtu ana mtazamo wake, na huwezi kulazimisha mtazamo wa mtu ubadilike.
Inasikitisha sana kuona mtu anayesambaza haya mambo ni bosi wangu, Bosi
wa mkoa wetu. Yeye akipiga mhuri kitu ndio imekaa hiyo, Yeye ana nguvu
zote,” amesema Ruge.
“Sasa
akisema hivyo mimi ni tapeli anataka kila mtu Dar es Salaam anione
hivyo. Mimi sina nguvu kwa hiyo nachagua kubaki kwenye ninacho kiamini.
Tangu mwanzo nilisema mimi nataka haya mambo yaishe, cha kusikitisha
huyu mtu ni kiongozi lakini anashindwa kumaliza jambo hili kwa busara na
anataka kuliendeleza.
“Kuna
mambo hapa yanajaribu kutengenezwa. Watu wanajaribu kutusukuma turudi
kwenye mjadala ambao tulishaumaliza. Mimi ni mtu mzima , na busara
inaniambia watu wazima hatuna haja ya kurudi kwenye majibizano ambayo
kwangu yaliisha siku nyingi “alieleza Ruge.