HII HAPA STORY YA MSICHANA ALIYEMKATA UUME MWANAUME ALIYEMBAKA KWA MIAKA MINGI
Mwanamke
mmoja nchini India amezikata sehemu ‘nyeti’ za mwalimu wa dini katika
jimbo la kusini la Keral kwa kudai kuwa alimbaka kwa miaka mingi.
Polisi
wamesema kuwa mtuhumiwa anayejulikana kama Gangeshananda Theerthapada
alikuwa akizuru katika nyumba ya mwanamke huyo ili kumfanyia matambiko
ya ibada baba wa mwanamke huyo aliyekuwa mgonjwa.
Mama
yake alikuwa na matumaini kuwa mtuhumiwa huyo aliyejidai kuwa mtakatifu
ataiondolea familia hiyo matatizo. Badala yake alikuwa akimbaka
msichana huyo mwenye miaka 23 kila anapotembelea nyumba hiyo.
Ijumaa
iliyopita alichukua kisu na kumshambulia alipojaribu kumbaka na baadaye
akaita maofisa wa polisi. Mbakaji huyo alikimbizwa hospitalini ili
kufanyiwa upasuaji wa dharura.