HUU HAPA UNDANI WA KIFO CHA MUME WA ZARI NYUMA YA PAZIA
Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika
Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga
‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria,
Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga
jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda,
katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na
ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery
Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo
usiku wa kuamkia juzi.
MARA YA MWISHO KUONEKANA
Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pati
ya Blankets and Wine iliyofanyika huko Kampala, Uganda wiki mbili
zilizopita. Ilielezwa kuwa, rais huyo wa Kundi la Rich Gang, mwenye umri
wa miaka 39, alionekana aliyedhoofu na asiyekuwa na furaha kama kawaida
yake huku akinywa soda na kula samaki, tofauti na alivyozoeleka kuwa ni
mtu wa kupiga vinywaji vikali, tena vya bei mbaya. “Nyuma ya hali yake
kiafya alionekana dhahiri mwenye matatizo yaliyosababisha hata kula yake
kuwa ya kusuasua na kusababisha hali kuwa mbaya zaidi,” kilikaririwa
chanzo hicho.
CHANZO CHA UGONJWA
Chanzo hicho kilidai kuwa, chanzo cha Ivan kupatwa na ugonjwa huo ni
pale alipotokea Sauzi na kwenda kuangalia moja ya mali zake (mashamba
makubwa) zilizopo Kampala na kukuta kuna watu wamebadilisha umiliki bila
yeye kujua. Ilisemekana kuwa, kuna wakazi waliotengeneza nyaraka na
hati za kumiliki ardhi ya jamaa huyo ambayo ilionesha walikuwa wamiliki
wapya ilihali ni mali ya jamaa huyo.
Wakati watu hao wakifanya hivyo, Ivan hakujua kilichokuwa
kikiendelea. Ilielezwa kwamba, ishu hiyo ilimsababishia Ivan mshtuko wa
moyo na maumivu makali ya kichwa ambayo pia yaliathiri utendaji wake wa
kazi wa kila siku.
Mbali na hilo, pia, kuliibuka taarifa za kuuzwa kwa nyumba yake na
watu wasiojulikana ambapo alitumia nguvu kubwa kukanusha taarifa hizo na
kueleza kuwa kwa utajiri alionao hawezi kuuza nyumba yake ya kifahari
iliyopo Munyonyo, Kampala.
“Mwishowe, alipoona hali yake kiafya inakuwa mbaya kutokana na
mshtuko uliotokana na mambo hayo, Ivan alichukua ndege na kwenda Afrika
Kusini kisha kuripoti mwenyewe katika Hospitali ya Steve Biko Academy
iliyopo Pretoria. “Vipimo vilionesha kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo
ambao ulisababishwa na kuganda kwa damu kwenye mishipa,” alisema sosi
huyo wa jijini Kampala. Mwishoni mwa wiki iliyopita, baba huyo wa watoto
watatu aliozaa na Zari alielezwa kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya
zaidi hivyo kufanyiwa operesheni kubwa ya kichwa.
ZARI ATHIBITISHA
Kupitia ukurasa wake Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Zari alithibitisha kifo cha mumewe ambapo aliandika
waraka wa simanzi: “Mungu huwapenda wale ambao ni maalum kwake ndivyo ulivyokuwa, umewagusa na kuwasaidia maelfu, ulifanya mengi ya kushangaza na nakumbuka maneno yako ‘maisha ni mafupi mno, acha tuishi kwa ukamilifu’. Hii ni saa ya giza, sasa naelewa kwa nini ulikuwa ukisema maneno hayo kwangu. “Kwa wanao, umekuwa shujaa -aina fulani ya superman. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa karibu yako anajua wewe ni mtu wa aina gani, anajua ucheshi wako.
waraka wa simanzi: “Mungu huwapenda wale ambao ni maalum kwake ndivyo ulivyokuwa, umewagusa na kuwasaidia maelfu, ulifanya mengi ya kushangaza na nakumbuka maneno yako ‘maisha ni mafupi mno, acha tuishi kwa ukamilifu’. Hii ni saa ya giza, sasa naelewa kwa nini ulikuwa ukisema maneno hayo kwangu. “Kwa wanao, umekuwa shujaa -aina fulani ya superman. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa karibu yako anajua wewe ni mtu wa aina gani, anajua ucheshi wako.
Watu watakumisi na kukumbuka sana kwa namna nyingi…Ulikuwa IVAN DON.
Baadhi ya mastaa wa Uganda walieleza ni namna gani walivyoshtushwa na
kifo cha Ivan. Bebe Cool –Natoa rambirambi zangu za dhati kwake na
familia yake. RIP kaka IVAN. Jose Chameleone -Mungu anaumba na kuchukua
kilicho chake! Mungu akurehemu rafiki yangu na kuimarisha familia yako
na sisi rafiki zako. Pumzika kwa amani Ivan. Ed Cheune –Ulieneza furaha
miaka yote ulipokuwa nasi wote, sasa ni zamu ya Mungu kukupa furaha yote
katika kurudi kwako kwake.
Pumzika kwa amani ndugu yangu mpendwa Ivan Semwanga. Baadhi ya mastaa
wa Kibongo walioandika mitandaoni kumlilia Ivan ni pamoja na Wema Isaac
Sepetu, Emmanuel Mbasha, Ali Kiba, Ester Kiama, Shilole na wengine
wengi kutokana na ukaribu wake na wao. Hadi gazeti hili linakwenda
mitamboni, bado utaratibu wa mazishi ulikuwa haujawekwa wazi. Ivan
alipata umaarufu Afrika Mashariki kutokana na biashara zake kubwa
ikiwemo umiliki wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini huku akisifika
kwa kusaidia shughuli za kijamii nchini Uganda.