Mbunge wa Vunjo, James Mbatia
(NCCR-Mageuzi) amekiri kumuahidi Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party,
sukari wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana na ameahidi
kutekeleza ahadi hiyo.
Mbatia alikiri kumwahidi Mrema sukari, lakini akaomba apewe muda wa wiki moja kutimiza ahadi yake.
Hatua ya Mbatia inatokana na hivi
karibuni Mrema kumshitaki kwa wananchi kuwa ameshindwa kutekeleza ahadi
alizoahidi wakati wa kampeni mwaka juzi.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa
NCCRMageuzi kitaifa, alichukua nafasi ya Ubunge wa Vunjo baada ya
kumshinda Mrema katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kwa mujibu wa Mrema, Mbatia alisema
katika kipindi hicho kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha
miundombinu ya jimbo hilo inakuwa sawa, lakini bado hajatekeleza ahadi
hiyo.
Kadhalika, Mrema alisema Mbatia amekuwa haonekani bungeni kwa kipindi kirefu kupeleka kilio cha wananchi.
Aliwataka wananchi wa Jimbo la Vunjo kutathmini kauli aliyoitoa Mbatia kuwa yeye Mrema ni mgonjwa ili wasichague kuwa mbunge.
JAMES MBATIA AKIRI KUMUAHIDI MREMA SUKARI NA AOMBA MUDA WA WIKI MOJA KUTIMIZA AHADI HIYO.
Reviewed by Unknown
on
7:09 AM
Rating: 5