Mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Beka Ibrozama anatarajia kuzindua bendi yake ‘Spidoch Band’
katika ukumbi wa Next Door uliopo Masaki jijini Dar es Salaam Aprili 29
mwaka huu.
Beka amesema kuwa
ametumia miaka mitatu kuandaa bendi hiyo ambapo alikuwa kimya kwenye
game la muziki kutokana na maandalizi hayo.
Pia mwanamuziki huyo
amesema kuwa amerudi tena kwa kushindo kwenye anga ya muziki kama
alivyofanya nyuma wakati akiwa katika jumba la kukuza vipaji nchini THT
akiwa na kina Barnaba, Amin na Lina.
Beka amedai alipokuwa
nje ya muziki alipata nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo
vitaboresha muziki wake kutokana na ukimya wake.
Aliongeza kwa kusema
kuwa alipotea kwa muda mrefu kimuziki kwa kuwa aliamua kujitolea muda
wake wote kwaajili ya kuandaa bendi yake.
Mwisho amewataka
mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo kwa ajili kuona
wanamuziki wake wapya ndani ya bendi hiyo.
BEKA IBROZAMA KUIZINDUA 'SPIDOCH BAND'APRILI 29.
Reviewed by Unknown
on
7:16 AM
Rating: 5