SIMULIZI YA KOSA LANGU:
AUTHOR : ADELA DALLY KAVISHE
Joyce ni msichana aliyezaliwa katika familia ya watoto wawili akiwa ni
mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Ndesanjo, maisha yao yalikuwa ni
maisha ya furaha na amani walikuwa wakiishi Mkoa wa Dar es salaam
maeneo ya Kimara Stop Over, lakini furaha hiyo ilipotea baada ya siku
moja ambapo Mzee Ndesanjo alikuja nyumbani baada ya kutoka kazini na
moja kwa moja akimtaka mama Joyce ajiandae kwani wangesafiri siku hiyo
ambapo ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya saa kumi na mbili jioni.Mzee
Ndesanjo alikuwa na gari aina Eskudo alifika na kuita kwa sauti "Mama
Joyce Mama Joyce" huko chumbani mama Joyce alimskia na kuitika "Bee
Mume wangu,vipi mbona unaonge kwa sauti sana si ungeingia ndani kwanza"
alisema mamaJocye huku akiwa anamuangalia mume wake kwa makini Baba
Joyce alimsogelea huku akisema "hakuna muda wa kupoteza mimi ndani
siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro kuna matatizo
kwani rafiki yangu tunayefanya naye kazi amefiwa na mke wake wake
inabidi tuwahi kwenda"
Mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari na
kusema "mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa
masikini" aliongea kwa masikitiko Baba Joyce akamjibu na kusema "alikuwa
anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke"
mama Joyce akasema "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani"
aliuliza mama Joyce kwani kwa wakati huo Jocye na mdogo wake aliyeitwa
James walikuwa wameenda shule Joyce alikuwa darasa la tano na James
akiwa darasa la kwanza na pale walipokuwa wakiishi likuwa ni nyumba ya
kupanga.Baba Joyce alimgeukia tena mke wake na kusema "hawa watoto
tutamkabidhi jirani yetu Mzee Ngonyani na mkewe kwani hatuendi kukaa
zaidi ya siku mbili wewe jiandae tuondoke wakirudi kutoka shule watakuta
maagizo kutoka kwa mke wa Ngonyani" alisema baba Joyce.
Ndipo mama Joyce akaenda kwenye chumba cha Mke wa Ngonyani na kumwachia
maagizo ya kuwaangalia watoto wake kwa kipindi cha siku mbili baada ya
hapo aliingia chumbani na kujiandaa tayari kwa safari ambapo safari
ilianza wakiwa njiani maeneo ya Kidatu ghafla gari lilipata pancha
tairi ya mbele na kupinduka ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani Baba Joyce
alifariki palepale na Mama Jocye alikuwa ameumia sana sehemu za
kichwani hivyo wasamaria wema walimchukua na kumkimbisa
hospitali,,,,nini kilitokea itaendelea....
ISOME HAPA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA INAITWA "KOSA LANGU"
Reviewed by Mipiko
on
3:01 AM
Rating: 5