Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli
amemuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance S. Mabeyo.
Zoezi la kuapishwa kwa mkuu huyo limefanyika, Jumatatu hii Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais Magufuli Alhamisi iliyopita
kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Devis Mwamunyange aliyestaafu.
Jenerali Mabeyo alikuwa Luteni Jenerali kabla ya kupandishwa cheo kuwa
Jenerali.
Wakati huo huo Rais Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi nchini, Luteni Jenerali James Mwakibolwa ambaye amechukua nafasi
iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo.
Hatimaye Jenerali Mabeyo Aapishwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi
Reviewed by Mipiko
on
2:41 AM
Rating: 5