Muda
mchache baada ya kusambaa kwa taarifa zinzomhusu mchezaji wa timu ya
vijana wa umri chini ya miaka 20 wa Mbao FC, Ismail Halfan, Shirikisho
la Soka nchini (TFF) limetoa taarifa kuhusu kifo cha mchezaji huyo.
“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kushtukiza cha Mchezaji Ismail
Halfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya
Mwanza kilichotokea leo Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba
mkoani Kagera.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama
vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba
katika Ligi ya vijana ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya
kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.
Ismail aliyeanguka uwanjani dakika
ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa
uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki
dunia.
Kamati ya Tiba ya TFF, bado
inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa
taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha
mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa
Kagera.
Inna Lillah wainna ilayhi Rajiuun. Mwenyezi Mungu, Subb Hanna Watallah ampumzishe mahali pema peponi roho ya marehemu huyu.”
Taarifa ya TTF kuhusu kifo cha mchezaji wa Mbao FC, Ismail Halfan
Reviewed by Mipiko
on
7:12 PM
Rating: 5