Davido Anena ya Moyoni...Adai hatoisahau Tanzania Daima
Ameufungua moyo wake kwenye post ya Diamond katika mtandao wa Instagram ya show yake ya mjini Harare nchini Zimbabwe – Watora Mari iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Kwenye post hiyo ya show hiyo iliyofana na kushuhudia akiujaza ukumbi mkubwa wa HICC akiwa na mwenyeji wake Jah Prayzah, Diamond aliandika: This Song Called #NumberOneRemix it has more than 18.5 Million Views on Youtube….. Go watch it and enjoy the Mix of Bongo flavour and Naija.”
Post hiyo ilimkuna Davido aliyeandika na kujibiwa na Diamond kama inavyoonekana hapo chini:
Kama ambavyo Jah Prayzah anamshukuru Diamond kwa kumtambulisha kwenye ramani ya muziki wa Afrika, Diamond atamshumkuru milele Davido kwa kumpa shavu kwenye remix ya Number One iliyompa staa huyo wa Tanzania umaarufu mkubwa.


