Chemsha
vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya
kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha
plastiki.
Hatua ya pili
Pima
vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha
sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko
huo uyeyuke.
Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa.
Hatua ya tatu
Taratibu
ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga
haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi.
Njia ya pili
Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C
Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo.
Baada
ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku
ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa
laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mbao
lilotangulizwa karatasi nyembamba la plastiki subiri saa 3 na sawazisha
sabuni kwa rula au kitu kingine kilicho nyooka huku ukigandamiza juu,
ipanguse iwe laini kwa kutumia kitamba kilicho lowanishwa.
Katakata
sabuni vipande kwa kipimo cha kuuza iweke ikauke katika sehemu yenye
kivuli kwa muda wa majuma 8 hadi 12 mfano- ndani ya chumba kwenye sakafu
iliyotandikwa kasha la karatasi nene.
Kwa Wajasiriamali wote....Fahamu Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA
Reviewed by Mipiko
on
7:02 PM
Rating: 5