Diamond Platnumz weekend hii amepost picha instagram akiwa
safarini na Mama yake kuelekea Afrika Kusini huku kwenye picha hiyo
akiwa ameandika ujumbe ambao unaonyesha huwenda mpenzi wake Zari
amejifungua.
Mapema mwezi uliopita katika hatua za kujiandaa na mapokezi ya mtoto
huyo, Zari alifanya baby shower nchini Afrika Kusini na kuwashirikisha
marafiki zake na watu wa karibu.
Jumapili hii Diamond akiwa safarini na mama yake kwenda Afrika Kusini, ameandika :
Na mama Chibu D Chibu De … flying to our new Second
home, South africa For my New Born… #MiniMe #ChibuJunior #YoungSimba
#YoungLion Ungependa nimpe jinangani eti?
Kama Zari amejifungua basi huyo ni mtoto wake wa pili na Diamond. Pia atakuwa mtoto wake wa tano kwa ujumla.
Diamond aandika ujumbe huu instagram akielekea SA akiwa na Mama yake...Awaomba mashabiki Jina la Mwanaye wa Pili
Reviewed by Mipiko
on
10:57 PM
Rating: 5