Mrithi wa "Scorpion" Huyu hapa...Anajulikana kama "Rambo" Mkatamapanga
Wiki chache baada ya kutokea kwa stori za ‘Scorpion’ ambaye alizichukua
headlines kutokana na kuhusishwa kwake na matukio ya uporaji na
kuwadhuru watu kadhaa kwenye maeneo ya Buguruni Jijini Dar es salaam,
Leo Heka Heka ya Clouds FM imekuja na stori nyingine ya Rambo mkata
mapanga.
Geah Habib kupitia Leo Tena ameipata stori hii ya jamaa anayefahamika
kwa jina la Rambo kutoka maeneo ya Karakata, Uwanja wa Ndege Dar es
salaam. Huyu jamaa inadaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwapora watu na
wengine kuwakata mapanga.
Wananchi wa maeneo hayo wamezungumzia vitisho ambavyo wamekuwa
wakivipata kutoka kwa Rambo ambaye aliwahi kufungwa jela na kuachiwa
wiki mbili mpaka tatu zilizopita. Wanawake wengi wameonesha kumuogopa
Rambo kwa madai kwamba anaweza kuwadhuru kwasababu hata wanaume zao
wamekuwa wakihofia kurudi nyumbani inapotokea wamechelewa kurudi au
wanarudi mapema ili kumkwepa.
"Yule mtu alifanya fujo mtaani akakamatwa, tangu kipindi cha Kova,
walimweka ndani lakini wamemuachia tena amerudi kutunyanyasa tena
wananchi. Sisi tunailaumu serikali kwanini wamemuachia, mtu amechoma
watu visu, amekata wanawake matiti, wanaume wenyewe wanamuogopa"-
Mwananchi
"Huyu Rambo ni shida na alianza haya mambo kitambo kidogo alikuwa
anakata watu mapanga kweli alikamatwa na polisi akapelekwa mahakamani
akahukumiwa kifungo. Lakini baadaye walikata rufaa akatolewa jela. Baada
ya kutoka jela akavamia watu akawakata mapanga watu eneo la shule ya
msingi Muhogo akachukua simu akaondoka nayo" – Diwani wa Sitaki Shari.


