Godbless Lema Afikishwa Mahakamani.......Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana

Lema amefikishwa leo mahakamani akiwa tayari amekaa rumande takribani siku 7 tangu alipokamatwa.
Lema
anakabiliwa na shtaka la uchochezi ambapo ni pamoja na kumtishia Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kauli yake aliyoitoa dhidi ya Rais
Dkt Magufuli kuwa Mungu amemuonyesha asipojirekebisha atafariki.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo, Lema amerejeshwa rumande baada ya kukosa
dhamana kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri.
Mahakama imeeleza kuwa itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya Lema Novemba 11 mwaka huu.



