Msanii wa muziki ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo
‘Binti kiziwi’, Z Anto amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa kuna label
zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji kufanya naye kazi lakini amekataa
kufanya nao kazi.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo kimya, amesema alipata ofa ya
kujiunga na WCB lakini alikataa kwa kuwa yeye mwenyewe anadai anatamani
kufanya kazi nje ya WCB.
“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka
saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo
sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati
ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha
kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na
maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi
natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip
Top Connection” Z Anto alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.
Akieleza sababu ya kukataa ofa ya kujiunga WCB, Z Anto alisema “Sisi
ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya kazi
sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo mengi
mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda
kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi
muda si mrefu,’ alisema Z Anto
Z Anto aeleza kwanini amekataa ofa ya kujiunga na WCB ya Diamond
Reviewed by Mipiko
on
5:03 PM
Rating: 5