Makamu wa rais
aliyefutwa kazi nchini Sudan Kusini Riek Machar, ambaye aliikimbia nchi
hiyo mwezi Agosti, ameapa kwamba atarejea nchini humo.
Amesema bado anapendwa na watu wa taifa hilo.
AKiongea
kutoka Afrika Kusini, Bw Machar ameambia BBC kwamba kundi lake la waasi
bado lina matumaini ya kuingia kwenye mkataba wa amani na Rais Salva
Kiir.
Amesema hayo licha ya mapigano makali kutokea mjini Malakal kati ya wanajeshi watiifu kwake na wanajeshi wa Rais Kiir.
Bw
Machar, ambaye baada ya kutoroka Sudan Kusini alikimbilia Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, na baadaye akaenda Khartoum, Sudan Kusini, kwa
sasa anapokea matibabu Johannesburg.
Mwezi Julai, walinzi wa Bw Machar na walinzi wa Rais Kiir
walipigana mjini Juba na kuanzisha vita vilivyodumu siku kadha na
kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Watu zaidi ya 100,000 walikimbilia nchi jirani.
Mapigano
hayo yalizuka chini ya mwaka mmoja baada ya mkataba wa amani uliokuwa
umetiwa saini wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kumaliza
vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Akiongea na kipindi cha HARDtalk cha BBC, Bw Machar amesema: "Nitarejea Sudan Kusini."
"Kwa sababu Rais Salva Kiir hataki uchaguzi huru na wa haki, ndio maana akatushambulia, alianzisha tena vita.
"Lakini
natumai kwamba viongozi wenye busara na hekima kutoka kanda hiyo, na
Afrika, na maeneo mengine ya dunia wataanzisha mchakato wa kisiasa ambao
utarejesha tena amani, na kufufua mkataba wa amani na kuundwa tena kwa
serikali ya mpito wa umoja wa kitaifa."
Bw Machar pia amekanusha
madai kwamba alichochea vita na badala yake akasema wanajeshi wake
walikuwa wanajilinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa wanajeshi wa
serikali.
Maafisa wa Rais Kiir wamewatuhumu wanajeshi wa Bw Machar kwa kuanzisha mashambulio hao.
Pande zote mbili zimetuhumiwa kwa kutekeleza uhalifu wakati wa vita.
Majuzi,
shirika la Amnesty International lilipendekeza kuundwe mahakama maalum
nchini humo ya kuchunguza waliotekeleza uhalifu wakati wa vita.
Machar aapa kurejea nyumbani Sudan Kusini
Reviewed by Mipiko
on
5:14 PM
Rating: 5