Mwanamfalme mmoja
nchini Saudi Arabia ameuawa kutokana na makosa ya kumuua mwanamume baada
ya mzozo miaka mitatu iliyopita mjini Riyadh, wizara ya mambo ya ndani
nchini humo imesema.
Hukumu ya kifo ilitekelezwa dhidi ya mwanamfalme huyo Turki bin Saud al-Kabir katika mji mkuu Riyadh.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu jinsi alivyouawa, lakini watu wengi waliohukumiwa kifo huuawa kwa kukatwa shingo.
Mwanamfalme
huyo ndiye mtu wa 134 kuuawa baada ya kuhukumiwa kifo nchini humo, kwa
mujibu wa orodha iliyoandaliwa na shirika la habari la AFP.
Lakini huwa nadra sana kwa watu wa familia ya kifamle kuuawa, wanahabari wanasema.
Mwanamfalme huyo alikiri kumuua raia huyo mwenzake, wizara ya mambo ya ndani imesema kupitia taarifa.
Wizara hiyo imewahakikishia raia kwamba serikali imejitolea "kudumisha usalama na kutekeleza haki".
Taarifa zinasema familia ya marehemu ilikataa malipo
ya kifedha kama fidia ili kutoitisha hukumu ya kifo dhidi ya
mwanamfalme huyo.
Kisa kinachofahamika zaidi cha mtu wa familia ya
kifalme kuuawa ni cha Faisal bin Musaid al Saud, aliyemuua mjomba wake,
Mfalme Faisal, mwaka 1975.
Wengi wa wanaouawa Saudi Arabia hupatikana na makosa ya mauaji au ulanguzi wa dawa.
Watu
karibu 50 hata hivyo waliuawa siku moja Januari kwa tuhuma za ugaidi,
akiwemo mhubiri maarufu wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr.
Mwanamfalme akatwa shingo Nchini Saudi Arabia
Reviewed by Mipiko
on
5:45 PM
Rating: 5