Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi auawa na polisi mkoani Kagera.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema mtu huyo Yahaya Leopard Kamuhanda alirusha bomu alilokuwa nalo mkononi wakati akikimbizwa na polisi pamoja na wananchi ambapo pamoja na kujeruhiwa watu hao, alikamatwa na kupigwa na wananchi ambapo kabla hajafa alieleza kuwa anamiliki silaha aina ya SMG nyumbani kwake katika kijiji cha Lukole Ngara, na polisi walifuatilia na kukuta bunduki moja aina ya SMG, magazine saba na risasi 275.
Amesema watu wanne waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni na kwamba kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya dola wanaendelea na msako wa wahalifu ambao walikuwa wakishirikiana nae.


