Hollande amtabiria ushindi Hillary Clinton katika uchaguzi wa Rais Marekani
Rais wa Ufaransa anaamini kuwa mwanamke ndiye atakayechaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
Akizungumzia kampeni za uchaguzi zinazoendelea nchini Marekani, Rais
Francois Hollande wa Ufaransa amesema kuwa kwa kuzingatia chunguzi
mbalimbali za maoni zilizofanyika nchini humo, tunaweza kutabiri kuwa
Hillary Clinton ndiye atakayeibuka na ushindi.
Hillary Clinton mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat
Rais wa Ufaransa ameongeza kuwa Ulaya haiwezi kuitegemea Marekani katika
kudhamini usalama wa mipaka yake, bila kujali kwamba Hillar Clinton
mgombea wa chama cha Democrat amekuwa na misimamo ipi au amefanya nini?
Kuhusu suala la kujiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, Rais wa
Ufaransa amesisitiza kuwa harakati huru za raia wa nchi za Ulaya huko
Uingereza ambazo ni moja ya misingi ya Umoja wa Ulaya hazipaswi
kutumbukia hatarini.Tafiti mbalimbali za maoni zinaonyesha kuwa Hillary
Clinton mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democrat
nchini Marekani anaungwa mkono na wapiga kura kwa asilimia 44 huku
Donald Trump mgombea wa chama cha Republican akiungwa mkono kwa asilimia
37. Uchaguzi wa Rais nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba 8
mwaka huu.


