DC KINONDONI AWATIA NDANI WATENDAJI KWA UZEMBE
wa
Mhe Hapi amesema, hatua
ya kuwaweka ndani watendaji hao na mkandarasi itawakumbusha juu ya
utekeleza wa miradi wanayotakiwa kusimamia na nini majukumu yao kwa
wananchi kwa madai kuwa uzembe umekithiri.
“Ofisi inapesa kwa miaka
miwili sasa ya kujenga Zahanati lakini wamekalia tu pesa hizo tangu
2014, pia miradi ya barabara na kushindwa kuweka polisi jamii ndani ya
kata hiyo licha ya kupewa maagizo kwa miezi 3 sasa hii ni dharau kwangu
na Rais aliye nituma” amesema
Aidha Hapi amewataka
watendani wote wa kata na maafisa ugani waliopo katika wilaya hiyo
kujiengua kwenye nyadhifa zao endapo wanaona hawawezi kuendana na kasi
inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano.
Lakini pia amemtaka mkuu
wa kituo cha polisi wa manispaa ya kinondoni kuwakamata watendaji kata
wote ambao hawajaunda vikundi shirikishi na kuwaweka ndani kwa muda wa
masaa 24 ili waweze kujieleza.


