IMETHIBITIKA:DIAMOND AMEKIRI KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA HAMISA MOBETO KUANZIA MWAKA 2009
Msanii mkubwa hapa Bongo Naseeb Abdul "Diamond Platinumz" amekiri kwamba amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo Hamisa Mobeto na kwamba mahusiano hayo yalianza kati ya mwaka 2009/10 kabla hata hajawa staa kama alivyo kwa sasa.
Mondi ameeleza hayo leo Jumanne kupitia kipindi cha Leo tena kinachorushwa kupitia Clouds fm na hii leo kimeruka mubashara pia kupitia Clouds tv. Diamond pia ameeleza mengi ikiwemo kashfa ya yeye kumkataa mtoto wa Hamisa na pia akaeleza kwa jinsi ambavyo familia yake imelichukulia jambo hilo.
Chibu ameeleza kwamba uhusiano wake na Hamisa Mobeto ulianza miaka ya 2009/10 wakati anatoka kimuziki na kipindi hicho alikuwa bado hajawa karibu na Wema Sepetu. Baadaye wawili hao waliachana na maisha yakaendelea kila mtu kimpango wake lakini kadri siku zilivyoenda Diamond alishawishika tena na ndipo mahusiano yao yakarejea na mwishowe Hamisa akajazwa ujauzito.
"Baada ya kuachana wakati mimi naendelea na maisha yangu na mpaka naanzisha mahusiano na Zari, ndipo shetani akanipitia na tukaanza tena kuwa na mawasiliano ya kimahaba mpaka Hamisa Mobeto alipopata ujauzito" amesema Diamond Platinumz.
Mondi amedai kuwa kutokana na yeye kuwa baba wa watoto wawili wa mke halali "Zari the Boss lady" alimwambia Mobeto kuwa suala la ujauzito wao lingetakiwa kubaki kubaki kama siri yao wawili na kwamba alikuwa akijitahidi kumpatia Mobeto matumizi ya kila siku. "Nilimuambia mimi ni baba mwenye familia yangu. Inabidi jambo hili libaki kati yangu mimi na wewe. Sikupenda kuikana mimba, ni damu yangu na kila siku iendayo kwa Mungu nilikuwa nampatia matumizi"



