PICHA:TAZAMA HAPA MEYA WA JIJI LA ARUSHA ALIVYOSHIRIKI KATIKA HAFLA YA KUWAPOKEA MANUSURA WA SHULE YA LUCKY VICENT
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Callist Lazaro akiimba wimbo wa Taifa katika hafla ya mapokezi ya manusura wa shule ya Lucky Vicent iliyofanyika juzi Ijumaa katika uwanja wa ndege wa KIA.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Callist Lazaro akijadiliana jambo na Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu katika hafla ya mapokezi ya manusura wa shule ya Lucky Vicent iliyofanyika juzi Ijumaa katika uwanja wa ndege wa KIA.
Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Mercy Masika naye pia alijumuika na wananchi uwanja wa ndege wa KIA katika mapokezi ya manusura hao, na hapo alikuwa akitumbuiza.
Kijana Wilson Tarimo ambaye ni mwiongoni mwa manusura wa shule ya Lucky Vicent akitoa neno la shukrani baada ya kupewa nafasi hiyo juzi Ijumaa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira ambaye pia alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hotuba pamoja na ujumbe wa serikali kuhusiana na tukio hilo kubwa.