MAJERUHI WA AJALI YA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT WAREJEA WAKIWA SALAMA
Watoto hao wakiwa wameshashuka kwenye ndege |
Furaha imetawala ujio wa watoto watatu wa Shule ya Lucky Vicent waliowasili leo Ijumaa, Agosti 18 wakitokea nchini Marekani kwenye matibabu baada ya kupata ajali Mei mwaka huu.
Wazazi na ndugu waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo kuwapokea watoto wao ambao wamepata nafuu kwa kiasi kikubwa.
Wilson Tarimo alikuwa wa kwanza kushuka katika ndege akiambatana na mdogo wake aliyeingia katika ndege kwa ajili ya kumpokea.
Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro akihutubia wananchi waliohudhruria tukio hilo |
Baada ya hapo aliyefuatia ni Saidia Awadhi pili akifuatana na Doreen Mshana kushuka katika ndege hiyo iliyokuwa na wajumbe 16 ambao waliambatana na watoto hao.
Baada ya kushuka walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliyeambata na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Arusha.