ZITTO KABWE ATOA SHUKRANI KWA RAIS MAGUFULI...NI BAADA YA RAIS KUAGIZA BARABARA YA KIGOMA-NYAKANAZI IJENGWE USIKU NA MCHANA
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo mheshimiwa Zitto Kabwe ameandika haya yafuatayo:-
"Mwaka 2015 kwenye uchaguzi Act Wazalendo tulikuwa na Ilani ya Mkoa wa Kigoma iliyokuwa na vipaumbele 10. Kipaumbele cha kwanza kilikuwa kuhakikisha kuwa Barabara ya Kigoma - Nyakanazi inajengwa Kwa lami. Pia katika ilani ya uchaguzi ya Kigoma Mjini tuliahidi kushirikiana Wabunge wote wa Kigoma kuhakikisha kuwa barabara Hii inajengwa. Wabunge wote wa Kigoma bila kujali vyama vyetu tumekuwa tukipigania Sana barabara Hii.
Jana tukiwa Kasulu Mjini Rais ameagiza zabuni ya barabara ya Kasulu- Kibondo itangazwe mwezi wa Agosti ili kupata wakandarasi wa kujenga barabara hiyo. Hii ni ahueni kubwa Kwa watu wa mkoa wa Kigoma. Tunamshukuru Sana Rais Kwa maagizo haya.
Barabara ya Kigoma - Nyakanazi imekuwa kilio chetu Kwa miaka mingi Sana. Wabunge wote wa Kigoma waliotangulia walikuwa wanahangaika na barabara Hii. Tunamshukuru mungu kwamba Sasa tumepata mradi huu".