Breaking News

TAZAMA ALICHOKIANDIKA MSANII LINAH BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

Msanii anayefanya vizuri kupitia tasnia ya bongo fleva jana aliripotiwa kujifungua mtoto wa kike katika hospitali ya Marie stopes iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.

Leo kupitia akaunti yake ya instagram Linah ameandika ujumbe ambao kwa kiasi kikubwa umedhihirisha kuwa tayari ameanza kulea. Ujumbe huo umeambatanishwa na picha ya viatu vya kike vya watoto huku ukisomeka "Mungu ni mwema kwangu".
A post shared by Linah Sanga (@officiallinah) on