Breaking News

ICHEKI HAPA RATIBA KAMILI YA NDONDO CUP HATUA YA ROBO FAINALI

Robo fainali ya Ndondo Cup inaendelea tena siku ya Alhamisi kwa timu nane kuumana katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Kinesi.
Droo hiyo iliyochezeshwa jana na kila timu kufahamu anapambana na nani katika hatua ya robo fainali iliweza kuwa ya aina yake baada ya watangazaji wa vipindi mbalimbali wa Clouds kugawana timu hizo na kuwapa ahadi lukuki .
Hii ndiyo Ratiba kamili ya Robo fainali.


Alhamisi 27/07/2017

Vijana Rangers vs Kibada one


Ijumaa Tar 28/07/2017


Goms United vs Mlalakuwa Rangers


Jumamosi Tar 29/07/2017


Mpakani Combine vs Misosi Fc

Jumapili Tar 30/07/2017

Keko Fanicha vs Stimutosha Fc


Leo tena wenyewe wamebaki na timu yao Mlalakuwa Rangers, kwa hiyo hawakuwepo kwenye draw ya kila kipindi kupata timu yake. XXL wao timu yao ni Keko Furniture, Jahazi wenyewe wameangukia kwa Mpakani Kombaini, Clouds 360 timu yao ni Misosi FC wakati amplifier watakuwa na Vijana Rangers, Kibada One wameangukia kwa Power Breakfast huku Goms United wakitua kwa Shilawadu na Stim Tosha ikienda kwa wazee wa Alasiri.

Baada ya droo hiyo kila kipindi kilitoa ahadi na mbwembwe kibao na kuziahidi timu hizo kuwa watanunua kila goli huku kipindi cha 360 wakitoa ahadi ya kuwapeleka mbuga za wanyama iwapo watakuwa mabingwa.Hello