BREAKING NEWS:RAIS MAGUFULI AFUNGUKA SABABU YA KUWATEUA MH. ANNA MGHWIRA NA PROF. KITILA MKUMBO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza sababu ya kuwateua viongozi wawili wa chama cha siasa cha ACT-Wazalendo kushika nyadhifa za juu serikalini.
Rais Magufuli ameyaeleza hayo leo Jumamosi alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika. Amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya kuwateua viongozi hao ni kuwa ameaona wana akili ya kutenda kulingana na kasi ya awamu hii ya tano.
Viongozi hao wa chama cha ACT-Wazalendo ni mheshimiwa Anna Mghwira ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na wa pili ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
"Nimemteua Prof. Kitila Mkumbo kwa sababu nimeona ana akili na ananifaa katika utendaji wangu...Nimemteua pia mama Anna Mgwira kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa sababu ana akili tofauti na hawa wengine....."
"Najua watu walihoji kwamba kwanini niteue kutoka ACT-Wazalendo tu na si vyama vingine???lakini nia yangu ni kuwa na watendaji watakaotekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi...."alisema Rais Magufuli.



